1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni siku ya pili ya mkutano wa makadinali na Papa Leo wa 14

8 Januari 2026

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo wa 14, anaendelea na mkutano wake wa dharura wa makadinali wote wa Kanisa Katoliki duniani ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe mwezi Mei mwaka jana.

https://p.dw.com/p/56U1q
Papa Leo XIV anasali Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa Leo XIV anasali Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu PetroPicha: Riccardo Antimiani/ZUMA/IMAGO

Tofauti na mikutano ya kawaida ya makadinali, ambayo inaweza kufanyika mara kadhaa kwa mwaka, mkutano huu wa dharura unawakutanisha si tu makardinali wanaoishi Roma, bali makadinali wote 245.Kwa mujibu wa tovuti ya Habari ya Vatican, ajenda zinajumuisha majadiliano kuhusu nyaraka mbili muhimu za mageuzi zilizotolewa na mtangulizi wa Papa Leo, Papa Francis aliyefariki dunia Aprili mwaka jana. Mpaka wakati huu, Vatican haijatangaza rasmi kile ambacho Papa Leo anakusudia kujadili na makadinali katika mkutano huo.