1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini kuongoza mkutano usio wa kawaida

26 Septemba 2023

Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini imesema nchi hiyo leo inaongoza mkutano usio wa kawaida na wanadiplomasia waandamizi kutoka Japan na China.

https://p.dw.com/p/4Wom6
Wanadiplomasia kutoka mataifa ya Korea Kusini, Japan na China katika picha ya pamoja
Wanadiplomasia kutoka mataifa ya Korea Kusini, Japan na China katika picha ya pamojaPicha: Yonhap News/picture alliance

Mkutano huo unaonekana kama juhudi za kujaribu kupunguza wasiwasi iliyonao China kuhusu kujiimarisha zaidi kwa Marekani katika mahusiano ya kiusalama na nchi hizo mbili, Japan na Korea Kusini. 

Soma pia:China yatangaza 'ushirikiano wa kimkakati' na Syria 

Mkutano huo utaangazia suala la uwezekano wa kuwepo ushirikiano kati ya serikali za mjini Seoul, Tokyo na Beijing na pia kutazama uwezekano wa kuanzisha tena mikutano ya viongozi wa juu kabisa iliyosimama kwa muda mrefu. Mara ya mwisho kufanyika mkutano wa aina hiyo ni mwaka 2019.

Kabla ya mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Park Jin, alisema ushirikiano baina ya nchi hizo tatu unabeba dhima muhimusio tu kwa eneo la kaskazini mashariki mwa Asia bali hata kwa uthabiti na maendeleo ya ulimwengu.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW