1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenyatta, Ruto wafuatilia mashitaka yao ICC

5 Machi 2013

Washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi za 2007-2008, Uhuru Kenyatta na William Ruto, wafuatilia kikao na mwisho cha Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kabla ya kuanza rasmi kwa kesi yao Aprili 10 na 11.

https://p.dw.com/p/17dsG
Former Kenyan Education Minister William Samoei Ruto sits in the courtroom of the International Criminal Court (ICC) in The Hague, Netherlands, Thursday, Sept. 1, 2011. Ruto is one of three senior Kenyan leaders appearing at the International Criminal Court for a hearing at which judges will decide whether evidence against them is strong enough to merit putting them on trial on charges of orchestrating deadly violence in the aftermath of disputed 2007 elections. (Foto:Bas Czerwinski/AP/dapd)
Kenia William Samoei RutoPicha: AP

Kenyatta na Ruto pamoja na mkuu wa zamani wa utumishi wa umma, Francis Muthaura, na mtangazaji wa redio, Joseph arap Sang, wanadaiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya miaka mitano iliyopita.

Tayari Muthaura na Arap Sang wameshakwenda mjini The Hague, lakini Kenyatta na Ruto wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho kwa njia ya mawasiliano ya vidio kutoka jijini Nairobi.

Ghasia hizo zilisababisha watu takriban 1,200 kuuwawa huku wengine zaidi ya 60,000 hadi leo wakiachwa bila makaazi. Kenyatta anapigania kuwa rais wa Kenya katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 4 Machi, huku Ruto akiwa mgombea wake mwenza.

Kuhusu kile hasa kinachojadiliwa katika kikao hicho, mwenzangu Amina Abubakar amezungumza na Abubakar Yusuf ambaye ni wakili nchini Kenya.

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Khelef