1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yaonya juu ya kitisho cha mashambulizi ya kigaidi

12 Oktoba 2023

Kenya imeonya juu ya kitisho kwamba makundi kama ya Al-Shabaab huenda yakafanya mashambulizi iliyoyaita ya mshikamano baada ya shambulizi la Hamas nchini Israel mwishoni mwa juma lililopita.

https://p.dw.com/p/4XT3C
Kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi nchini Kenya kimesema kupitia ukurasa wao wa mtandao wa X (awali ukijulikana kama Twitter) kwamba, mgogoro kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas unaathiri usalama wa ulimwengu mzima.
Kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi nchini Kenya kimesema kupitia ukurasa wao wa mtandao wa X (awali ukijulikana kama Twitter) kwamba, mgogoro kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas unaathiri usalama wa ulimwengu mzima.Picha: Hassan Ali ElmiAFP/ Getty Images

Taifa hilo la Afrika Mashariki limekabiliwa na mashambulizi kadhaa makubwa ya kigaidi yaliyofanywa na kundi la Al-Shabaab la nchini Somalia, tangu ilipopeleka wanajeshi nchini humo mwaka 2011 kukabiliana na wanamgambo hao wanaofungamana na al-Qaeda.

Idara ya polisi ya kupambana na ugaidi nchini Kenya imeandika katika mtandao wa X juu ya kitisho hicho na kuwaomba Wakenya kuwa waangalifu na kuripoti shughuli za kigaidi ili wachukue hatua.

Wizara ya mambo ya nje ya Kenya siku ya Jumamosi ililaani vikali shambulizi hilo la Hamas dhidi ya watu wa Israel.