Kasisi achomwa kisu Uturuki | Habari za Ulimwengu | DW | 17.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kasisi achomwa kisu Uturuki

IZMIR

Kasisi wa Kikatoliki amechomwa kisu katika mji wa magharibi mwa Uturuki wa Izmir.

Polisi imesema kasisi huyo Adriane Francini ameshambuliwa kwenye kanisa la St. Antoine lakini maisha yake hayako hatarini.Shirika la habari la Anatolia limeripoti kwamba mashambuliaji mwenye umri wa miaka 19 alikamatwa muda mfupi baadae.Mtuhumiwa huyo ameiambia polisi kwamba aliwasiliana na kanisa hilo kutokana na udadisi na kwamba kanisa lilimkaribisha ahudhurie misa. Hili ni shambulio jipya katika mfululizo wa mashambulio dhidi ya Wakristo nchini Uturuki nchi ya Kiislam ambayo inajivunia kwa msimao wake wa kutoegemea dini yoyote ile.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com