JOHANNESBURG:Watoto laki moja huzaliwa wakiwa wana virusi vya HIV kila mwaka | Habari za Ulimwengu | DW | 10.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANNESBURG:Watoto laki moja huzaliwa wakiwa wana virusi vya HIV kila mwaka

Shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF limesema takriban watoto laki moja nchini Afrika Kusini wanazaliwa wakiwa wameambukizwa virusi vya HIV na idadi nusu ya watoto hao hufariki kabla ya kufikisha umri wa miaka miwili.

Shirika la UNICEF katika ripoti yake limeeleza kuwa watoto wanaondelea kuishi hukabiliwa na maisha magumu katika jitihada za kuishi na ugonjwa wa UKIMWI.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com