1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jitihada za Tanzania kutokomeza ukeketaji

11 Novemba 2021

Serikali ya Tanzania imeanzisha mkakati wa kitaifa wa kutokomeza vitendo vya kikatili vya ukeketaji watoto wa kike, mkakati ambao pia unawajumuisha wahusika wa vitendo hivyo kama vile viongozi wa kimila. 

https://p.dw.com/p/42sWi
Uganda - Uganda - Improvisiertes Werkzeug ehemals genutzt zur Genitalverstümmelung
Picha: Getty Images/AFP/Y. Chiba

Mila potofu ya kuwakeketa mabinti bado inaonekana kuwa donda ndugu na maeneo kama vile kanda ya ziwa ikihusisha mikoa kama Mara, Shinyanga, Simiwi  na mikoa mingine ya jirani ikiwamo Singida matukio ya namna hiyo bado yako juu na wakati mwingine hufanyika kwa usiri kohofia rungu la dola.

Wanaofanya vitendo hivyo wanamini wako katika mkondo unaotambulisha mila na utamaduni , lakini kwa kutizama ukweli wa mambo, vitendo hivyo vinapora na kuutezwa utoto wa kike.

Mtoto wa kike aliyekeketwa kama anavyosema  Naibu Waziri wa Afya, Mwanaidi Ali Khamis anapoteza thamani mbele ya uso wa jamii na kwa maana hiyo ile ndoto yake ya kufika mbali inapita kwenye mawimbi na misuko suko.

Wengi wanasema kwamba jamii iliyostarabika haiwezi kamwe kutupa wala kusau utamaduni wake, lakini utamaduni unaoonekana kufifisha maisha ya kundi fulani ya watu ni umaduni uliopotea njia. 

Kulingana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu kuna mambo mengi jamii inaweza kuendelea kuvirithisha vizazi vyake kama vile masuala ya jando na unyago mambo ambayo humwandaa kijana kwa maisha ya baadaye, lakini ukeketaji ni utamaduni uliopitwa na wakati.

Symbolbild FGM
Ngariba hutumia vifaa duni kuwakeketa wasichanaPicha: picture alliance/dpa/EPA/UNICEF/HOLT

Kampeni hii ya kitaifa ina shabaha ya kuwafungua macho wale wanaoendelea kukumbatia vitendo hivyo kugutuka ili hatimaye washiriki juhudi za pamoja kumsaidia mtoto wa kike kukua katika malezi mema huku akiendelea kufurahia masomo.

Kwa vile elimu ni ufunguo wa maisha, bila shaka mangariba wanatajwa kuwa nyuma ya ukeketaji huo wanaweza kufuata uamuzi uliochukuliwa na ngariba mwenzao kama huyu ambaye sasa hayuko tena huko.

Tafiti nyingi zilizofanywa katika miaka ya hivi karibuni zinaonyesha hatua kubwa imepigwa kuwafungua wananchi juu ya mili hizo potufu,ingawa safari bado ni ndefu.

Vita dhidi ya utamaduni wa kuwakeketa wasichana katika jamii ya Wamaasai

Shirika la Amref ambalo linajiweka karibu na masuala ya afya, linasema katika uchunguzi wa kitafiti uliofanywa mwaka 1996 inaonyesha kiwango cha ukeketaji kilifikia asilimia 18 lakini katika utafiti wake mwingine wa mwaka 2015-2016 kiwango hicho kilipungua kikionyesha kwamba msichana mmoja kati 10  alikeketwa.

Kama wasemavyo wahenga, wimbo wenye waitikiaji wengi unafikisha ujumbe kirahisi, bila shaka juhudi hizi za pamoja zitasaidia kuwaamsha wale wanaoendelea kukumbatia mila hizo kutambua kuwa sasa zimepitwa na wakati.