1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel imejitayarisha kupambana na shambulizi la Iran

Amina Mjahid
7 Aprili 2024

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema nchi yake iko tayari kupambana na hatua yoyote itakayochukuliwa na adui yake Iran baada ya majenerali wake saba kuuwawa katika shambulio linaloaminika kufanywa na Israel

https://p.dw.com/p/4eVw3
Israel Tel Aviv
Waziri wa Ulinzi wa Israel Joav Galant,Picha: Abir Sultan/AP Photo/picture alliance

Gallant ametoa tamko hilo baada ya kufanya tathmini ya kiusalama na maafisa wakuu wa jeshi na kuweka mikakati ya kulipiza kisasi iwapo watashambuliwa na Iran. 

Iran kupitia Mnadhimu wake Mkuu wa jeshi Jenerali Mohammed Bagheri iliahidi kujibu shambulio linalodhaniwa kutoka Israel lililovurumishwa mjini Damascus Syria, lililosababisha mauaji ya majenerali saba wa Iran akiwemo kamanda wao mkuu. 

Marekani yajitayarisha na kitisho cha shambulizi la Iran

"Wakati, aina na mpango wa operesheni yetu ya kulipiza kisasi itaamuliwa na sisi wenyewe, katika njia ambayo watajuta walichokifanya. Hili bila shaka litafanyika," alisema Bagheri.

Israel hata hivyo haijathibitisha kuhusika na shambulizi hilo.