Israel yamkosoa waziri wa ulinzi wa Pakistan kabla mkutano
10 Aprili 2026
Matangazo
Asif alikuwa ameielezea Israel kama ovu, laana kwa ubinadamu na taifa la saratani katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa X Alhamisi, akiishutumu kwa kutekeleza mauaji katika Ukanda wa Gaza, Iran na Lebanon, na kusema anatumai wale waliohusika na kuunda dola hilo watateketezwa jehanamu.
Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu iliyaita matamshi ya Asif kuwa ya kuchukiza ikisema hakuna serikali inayopaswa kuvumilia matamshi kama hayo hasa ile inayofanya kazi kama mpatanishi asiyeegemea upande wowote.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema ana matumaini makubwa kuhusu uwezekano wa kufikia makubaliano na Iran kabla ya mazungumzo ya mwishoni mwa wiki hii mjini Islamabad, Pakistan.