Iran yatishia usalama wa bandari za Mashariki ya Kati
13 Aprili 2026
Shirika la habari la Tasnim limemnukuu msemaji wa uongozi wa jeshi hilo akisema kuwa vizuizi vya usafiri wa meli katika maji ya kimataifa ni hatua isiyo halali.
Msemaji huyo pia amesisitiza kuwa usalama wa bandari katika eneo la Ghuba ya Uajemi na katika bahari ya Oman aidha ni wa kila mtu ama ni hatari kwa wote.
Mapema leo, jeshi la Marekani lilitangaza kuanza kuweka mzingiro kwenye bandari zote za Iran na maeneo ya pwani, huku Rais Donald Trump akitafuta kuishinikiza Iran katika hatua ambayo inahatarisha kupanda kwa bei ya mafuta duniani na kuzua upya vita.
Wakati huo huo, viongozi mbali mbali wa dunia wameendelea kutoa maoni yao kuhusu mazungumzo ya amani Marekani na Iran ya kutafuta suluhisho yaliyokamilika mjini Islamabad bila makubaliano.
Baadhi ya viongozi wameelezea kuwa bado wana imani na mchakato huo wa amani huku wengine wakionyesha kukatishwa tamaa.