1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaimarisha mashambulizi katika matafa ya Ghuba

Josephat Charo
20 Machi 2026

Mataifa ya Ghuba leo yaliripoti mashambulizi zaidi kutoka Iran, huku Tehran ikiendelea kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Israel na Marekani.

https://p.dw.com/p/5AlXc
Kiwanda cha kusafishia mafuta cha Kuwait kimeshambuliwa na Iran.
Kiwanda cha kusafishia mafuta cha Kuwait kimeshambuliwa na Iran.Picha: AP Photo/picture alliance

Mataifa ya Ghuba yaliripoti mashambulizi zaidi kutoka Iran, huku Tehran ikiendelea kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Israel na Marekani.

Kiwanda cha kusafishia mafuta cha Kuwait kimeshambuliwa na droni ya Iran mapema leo Ijumaa na ving'ora nchini Israel vimetahadharisha juu ya mashambulizi huku milipuko ikisikika katika anga la Tehran kutokana na mashambulizi ya kutokea angani ya Israel, wakati Iran ikisherehekea Mwaka Mpya wa Kiajemi, Namruz.

Kuwait imesema mawimbi mawili ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika kiwanda chake cha kusafisha mafuta cha Mina Al-Ahmadi yalisababisha moto na waokoaji walikuwa wakifanya kazi ya kuudhibiti moto huo.

Kiwanda hicho cha kusafisha mafuta, ambacho kinaweza kusindika mapipa 730,000 ya mafuta kwa siku, tayari kilikuwa kimeharibiwa jana Alhamisi katika shambulio lingine la Iran.

Milipuko mikubwa pia ilisikika huko mjini Jerusalem baada ya jeshi la Israeli kuonya kuhusu makombora ya Iran yaliyovurumishwa kuelekea nchini humo.