1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC: Ukatili wa El Fasher huenda ukawa uhalifu wa kivita

3 Novemba 2025

Ofisi ya Mwendesha mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imeonya kuwa ukatili unaofanyika katika mji wa El Fasher Sudan, unaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

https://p.dw.com/p/5317L
The Hague 2025 | Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICCPicha: Piroschka van de Wouw/REUTERS

Ofisi ya Mwendesha mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imeonya kuwa ukatili unaofanyika katika mji wa El Fasher Sudan, unaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Ofisi hiyo imesema ina wasiwasi kuhusu mauaji ya halaiki, ubakaji na uhalifu mwengine unaodaiwa kufanyika katika mji huo ulioko katika mkoa wa Darfur Magharibi.

Baada ya miezi 18 ya kuuzingira mji huo, mashambulizi na njaa kali, wanamgambo wa RSF waliudhibiti Oktoba 26 baada ya kuwa mikononi mwa vikosi vya usalama. El Fasher ndio ngome ya mwisho kubwa zaidi iliyokuwa inashikiliwa na vikosi hivyo.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 65,000 wameukimbia mji huo, huku wengine 5000 wakihamia katika mji jirani wa Tawila lakini maelfu ya wengine wengi bado wamekwama katika mji huo unaokumbwa na vita.