Hu Jinatao amaliza ziara yake Tanzania. | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.02.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hu Jinatao amaliza ziara yake Tanzania.

Aelekea Mauritius kituo cha mwisho cha ziara yake Afrika.

default

Rais Hu Jintao wa China.

Rais Hu leo(Jumatatu) ,baada ya ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania. Akiwa Tanzania alisaini mkataba wa msaada na zaidi ya dola milioni 21 .

Mauritius ni kituo cha nne na cha mwisho cha ziara ya kiongozi huyo wa China katika bara la Afrika, ambapo ameshazizuru Mali,Senegal na Tanzania alikomaliza ziara yake leo asubuhi.Akiwa nchini humo Rais Hu Jintao alisaini mikataba ya msaada na mikopo ya zaidi ya dola milioni 21 mbali na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete.

Miongoni mwa miradi itakayonufaika na msaada huo wa China ni pamoja na matumizi ya dola milioni 4.4 milioni kwa ajili aya kukarabati vituo vya serikali vya matangazo ya radio na televisheni katika visiwa vya Zanzibar China pia imekubali kutuma wafanyakazi wa kujitolea kusaidia katika nyanja mbali mbali nchini Tanzania na ikiwemo huduma ya afya.

Kubwa zaidi wakati wa ziara hiyo ni kufunguliwa kwa uwanja mkubwa wa michezo mjini Dar es salaam uliojengwa na wachina kwa gharama ya dola milioni 56 na ambao ni wa aina yake katika Afrika mashariki na kati.

Ziara ya kiongozi huyo ina lengo la kuimarisha uhusiano wa China na bara la Afrika pamoja na kuinua haiaba yake katika bara hilo. Rais Ki´kwete alisema China na Tanzanaia zinamsimamo wa pamoja katika masuala mengi na hasa ya maendeleo na amani duniani. Aidaha alisisitiza pia kwamaba nchi zote mbili zinataka kuona mazungumzo ya biashara ya Doha yanakamilishwa haraka, jambo amabalo alisema ni la manufaa kwa nchi zianazoendelea.

Kwa upande wake Bw Hu alisema China imevutiwa sana na Tanzania kwa mchango wake katika kuleta amani na kutanzua migogoro barani Afrika na hasa katika nchi za jirani.

China ni moja kati ya wawekezaji 10 bora nchini Tanzania.Kwa jumla katika ziara yake hii ya nchi nne barani humo, Rais Hu Jintao atakua ametia saini mikataba ya misaada na mikopo inayogharimu zaidi ya dola milioni 100.

Wakati China ikijiimarisha kiuchumi barani Afrika, imekosolewa vikali kwa kuyafumbia macho masuala ya uongozi kama demokrasia, utawala bora na haki za binadamu katika nchi husika.

Mohamed AbdulRahman/RTR

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com