Hija ni ibada takatifu ya Kiislamu inayofanyika kila mwaka katika miji mitakatifu ya Makka na Madina nchini Saudi Arabia. Ni nguzo ya tano ya Uislamu ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kuifanya alau mara moja.