Mecca, Saudi Arabia. Hija inaanza leo. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mecca, Saudi Arabia. Hija inaanza leo.

Nchini Saudi Arabia , karibu watu milioni 2 waumini wa dini ya Kiislamu wameanza Hija ya kila mwaka katika mji wa Mecca.

Wakiwa wamevaa nguo nyeupe , mahujaji walitembea ama walipanda mabasi kwenda katika bonde la Mina , kiasi cha kilometa tano mashariki ya Mecca, kuanza kufuatilia safari iliyofanywa na Mtume Mohammad zaidi ya miaka 1,400 iliyopita.

Maelfu kadha ya wanausalama wa Saudi Arabia wamewekwa katika maeneo mbali mbali yatakayotumika na mahujaji na maafisa wanaonya kuwa watazuwia jaribio lolote la kuharibu hali ya usalama wakati wa Hija. Hija iliyopita ilichafuliwa na mkandagano ulioleta maafa ambapo watu 364 waliuwawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com