Shughuli za Hijja za mwaka huu zafikia ukingoni | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Shughuli za Hijja za mwaka huu zafikia ukingoni

MINA:

Sherehe za Hijja za mwaka huu ndio zinafikia kikomo leo.Kundi la mwisho la mahujai wapatao millioni 2 unusu,limefanya shughuli ya kutupa mawe katika nguzo kama ishara ya kupiga shetani.Mahujajo hao baada ya kutupa mawe katika nguzo hizo wameanza kurejea Makkah kabla ya kuanza safari ya kurejea makwao.

Hakuja ripotiwa majeruhi ama vifo kutokana na mkanyagano katika sherehe za mwaka huu.Katika hija zilizopita kumekuwa na visa vya watu kupoteza maisha wakati mwingine katika mkanyagano wakati baadhi ya mahujaji wakijaribu kusogelea nguzo hizo kwa ajili ya kutupa mawe.

Januari mwaka wa 2006 watu 364 waliuliwa wakati wa kupiga mawe na tukio lingine lilitokea mwaka wa 2004 ambapo watu 251 kupoteza maisha yao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com