1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saud Arabia yaahidi uchunguzi wa kina

25 Septemba 2015

Zaidi ya mahujaj 700 wameuwawa na mamia kujeruhiwa kufuatia vurumai na mkanyagano huko Mina.Huo ni msiba mmojawapo mkubwa kabisa kutokea wakati waumini wa dini ya kiislam wanapotekeleza nguzo ya tano ya dini yao.

https://p.dw.com/p/1GdT1
Waumini wakifanya ibada Karibu na mlima Arafat nje ya MaccaPicha: Reuters/A. Masood

Ni msiba mkubwa kabisa kuwahi kugubika Hijja tangu miaka 25 iliyopita.Mahujaj zaidi ya milioni mbili wamekusanyika mwaka huu.

Mfalme Salman aliyekutana na wakuu wa maandalizi ya Hajj amesema anasubiri haraka matokeo ya uchunguzi,na kuongeza ameamuru mipango ya maandalizi ya Hijja idurusiwe ili kuhakikisha waumini wanatekeleza salama kabisa wajib wao kuambatana na nguzo ya tano ya dini ya kiislam.

"Bila ya kutilia maanani matokeo ya uchunguzi,juhudi za kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa Hajj hazitosita.Tumezitaka taasisi husika zidurusu sera zao na jinsi ya kutoa dhamana."Amesema mfalme huyo.

Akizungumzia hapo awali kuhusu ajali hiyo,waziri wa afya wa Saud Arabia Khaled al Faleh aliwalaumu kwanza mahujaj kwa kile alichokitaja kuwa "kutotilia maani muongozo..Lakini msemaji wa wizara ya mambo ya ndani,jenerali Mansur Turki alionekana kuwa na tahadhari zaidi aliposhauri watu wasiharakishe kusema kitu kabla ya matokeo ya uchunguzi kutangazwa.Amesema tu "joto kali na kuchoka sana mahujaj vimechangia kuifanya idadi ya wahanga iwe kubwa mno.

Walimwengu waelezea huzuni zao

Wakati huo huo walimwengu wanaomboleza.Ikulu ya Marekani,katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon,serikali kuu ya Ujerumani,Ufaransa,mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Ulaya,Donald Tusk na Uturuki wametuma rambi rambi zao kutokana na msiba huo.

Saudi-Arabien Hadsch Massenpanik in Mina
Wauguzi wakiwahudumia majeruhi wa Mkaganyagano wa MinaPicha: Reuters/Stringer

Katika wakati ambapo wengi wa mahujaj ni wageni,Iran imesema mahujaj wake wasiopungua 131 wamefariki kufuatia ajali hiyo.Kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei amewatwika jukumu la ajali hiyo viongozi wa Saud Arabia na kukosoa "usimamizi mbaya."

Usimamizi wa Hija wakosolewa

Lawama kama hizo zinatolewa pia na mahujaj wanaosema wanaogopa kuendelea kuhiji.Mohammed Hassaan,raia wa Misri mwenye umri wa miaka 39,anasema anaogopa kuendelea kuhiji,isije ikatokea ajalai nyengine ya msukumano leo hii,akitaja pia usimamizi mbaya wa pirika pirika za mahujaj zaidi ya milioni mbili waliokusanyika Mina,kilomita chache kutoka Macca.

Saudi Arabien Hadj Mina Steinigung Satan Pilger Mekka Eid al-Adha
Mahujaj wanaendelea kumtupia mawe shetaniPicha: Reuters/Ahmad Masood

"Saud Arabia inatumia fedha nyingi kwaajili ya Hijja,lakini maandalizi yana kasoro"amesema hujaj mwengine,Ahmed wa kutoka Misri.

Licha ya hofu lakini,waumini waliodhamiria kukamailisha nguzo ya tano ya dini ya kiislam,wanaendelea hii leo kumtupia mawe shetani.

Hujaj mmoja wa kutoka Syria anasema anaendelea na Hijja kwasababu tunanuku " Mungu anawalinda."

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP/AP

Mhariri:Yusuf Saumu