MAKKAH: Hija yaendelea kama ilivyopangwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 29.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MAKKAH: Hija yaendelea kama ilivyopangwa.

Serikali ya Saudi Arabia imesema Hija ya mwaka huu inaendelea kama ilivyopangwa.

Takriban Waislamu milioni mbili wamo mjini Makkah kwa muda wa siku tano kwa ibada ya kujitakasa na dhambi.

Hija ya mwaka huu inatekelezwa wakati ambapo kuna hali ya taharuki kati ya waislamu wa madhehebu ya Sunni na wale wa madhehebu ya Shia.

Hata hivyo maafisa wa serikali ya Saudi Arabia wameotahadharisha watakabiliana vikali na watu watakaotatiza usalama wakati wa Hija.

Maelfu ya maafisa wa usalama wamewekwa mabarabarani, huku zahanati na vituo kadhaa vya afya vikijengwa katika eneo hilo.

Hija ya mwaka uliopitwa ilikumbwa na mkasa ambapo watu 364walifariki baada ya mkurupuko.

Mwaka 2004 watu zaidi ya 250 waliuawa kwenye mkurupuko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com