1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haiti inapanga kufanya uchaguzi wake Agosti 2026

3 Desemba 2025

Haiti iliyoathiriwa na magenge imepiga hatua kuelekea kufanya uchaguzi wake wa kwanza katika takriban muongo mmoja baada ya mamlaka kutangaza kwamba nchi hiyo ya Caribbean itafanya uchaguzi majira ya kiangazi yajayo.

https://p.dw.com/p/54ezr
Haiti Belladere 2022 | Kufukuzwa kwa Wahaiti mpakani na Jamhuri ya Dominika
Kijana anatazama lori la uhamiaji likiwabeba Wahaiti waliorejeshwa na Jamhuri ya Dominika katika mpaka wa Dominika na Haiti, Belladere, Haiti, tarehe 17 Desemba 2022.Picha: Richard Pierrin/AFP/Getty Images

Duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu inatarajiwa kufanyika Agosti 2026, lakini kurejesha usalama kote Haiti ni muhimu kwa ajili ya uchaguzi, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Muda, chombo kilichotoa amri hiyo na kinachohusika na kuandaa uchaguzi. Mwenyejiti wa tume hiyo Jacques Desrosiers amenukuliwa akisema "Kurejesha usalama ni sharti la awali kwa kufanyika kwa duru ya kwanza” ya uchaguzi wa bunge na urais. Kwa muda mrefu haiti imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kisiasa na kiusalama, na hali imezidi kuwa mbaya tangu mapema mwaka 2024, wakati aliyekuwa waziri mkuu Ariel Henry alilazimishwa kujiuzulu na magenge yenye silaha ambayo bado yanadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu Port-au-Prince.