1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghana: Senegal isaidie kutatua mizozo ndani ya ECOWAS

18 Mei 2024

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo amemtaka mwenzake wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, kutumia utashi wake ndani ya Jumuiya ya ECOWAS ili kusaidia kutatua mizozo iliyopo.

https://p.dw.com/p/4g1NJ
Rais wa Senega Bassirou Diomaye Faye
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye FayePicha: Luc Gnago/REUTERS

Rais Akufo-Addo amemtaka Faye, kusaidia kutatua mzozo kati ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS na mataifa ya Niger, Burkina Faso na Mali.

Mataifa hayo matatu yalitangaza mnamo Januari mwaka huu kujiondoa kwenye Jumuiya hiyo baada ya kuchukuliwa hatua ya kusitishwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi.

Soma pia:Rais wa Senegal afanya ziara ya kwanza nchini Nigeria

Rais Faye amewasili katika mji mkuu wa Ghana, Accra mapema leo asubuhi baada ya kumtembelea Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu. Rais Faye amesema Jumuiya ya ECOWAS, ambayo Tinubu ni mwenyekiti wake, inapitia wakati mgumu lakini bado kuna matumaini. Nigeria na Senegal zimeahidi kukuza demokrasia katika eneo la Afrika Magharibi.