1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yasimamisha Visa za zaidi ya mara kwa raia wa Urusi

7 Novemba 2025

Nchi za Umoja wa Ulaya hazitatoa tena viza za kuingia zaidi ya mara moja katika mataifa ya Umoja huo kwa raia wa Urusi, kufuatia "vitendo vya hujuma na uwezekano wa matumizi mabaya" ya viza hizo.

https://p.dw.com/p/53HDL
Ubelgiji Brussel 2025 | Kaja Kallas
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Ulaya, Kaja KallasPicha: Nicolas Tucat/AFP

Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imesema raia wa Urusi watalazimika kuomba viza mpya kila wanapotaka kuingia Ulaya kwa lengo la kuwachunguza mara kwa mara waombaji wa viza hizo ili kupunguza uwezekano wa hatari.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wajenga mazingira hatari

Katika taarifa, mjumbe maalumu wa Umoja huo Kaja Kallas, amesema kwa miongo kadhaa, uvamizi haramu wa Urusi dhidi ya Ukraine umejenga mazingira hatari zaidi ya usalama Ulaya.

Pia amesema kwa sasa wanakabiliwa na usumbufu wa droni na hujuma kwenye ardhi yao kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

Kallas pia amesema ni jukumu la Umoja huo wa Ulaya kuwalinda raia wao.