1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

EU kutoa msaada wa euro milioni 458 Mashariki ya Kati

16 Machi 2026

Umoja wa Ulaya umetangaza kutoa msaada wa kibinadamu wa euro milioni 458, sawa na dola milioni 526, kwa nchi za Mashariki ya Kati mwaka 2026.

https://p.dw.com/p/5AUzi
Brussels 2026 |  Hadja Lahbib
Kamishna wa usimamizi wa majanga wa Umoja huo, Hadja Lahbib, Picha: Valentine Zeler/European Union

Kamishna wa usimamizi wa majanga wa Umoja huo, Hadja Lahbib, amesema hatua hiyo inaonesha ni kwa jinsi gani EU inaongeza juhudi zake kusaidia waathiriwa wa migogoro, wakati wadau wengine wakipunguza mchango wao.

Kati ya fedha hizo, euro milioni 210 zitatolewa kusaidia raia nchini Syria kwa mahitaji kama chakula, huduma za afya, makazi, maji safi na elimu kwa watoto waliokosa masomo. Takwimu za Umoja wa Ulaya zinaonyesha kuwa watu milioni 16.5 Syria wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Aidha, euro milioni 124 zitatolewa kusaidia mahitaji ya msingi katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, huku euro milioni 100 zikitengwa kwa msaada wa kibinadamu nchini Lebanon.

Fedha nyingine euro milioni 15.5 zitaelekezwa Jordan na euro milioni 8 nchini Misri kusaidia juhudi za misaada ya dharura.