1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUmoja wa Falme za Kiarabu

Dubai, Kazakhstan na Urusi zashuhudia mafuriko makubwa

17 Aprili 2024

Mtu mmoja amekufa baada ya gari lake kusombwa na maji huko Ras Al Khaima kufuatia mafuriko yaliyoripotiwa huko Dubai.

https://p.dw.com/p/4esWz
Mafuriko yashuhudiwa Dubai
Mafuriko yashuhudiwa DubaiPicha: Jon Gambrell/AP/dpa/picture alliance

Katika maeneo mengine takriban watu 117,000 wamehamishwa nchini Kazakhstan kutokana na mafuriko katika taifa hilo la Asia ya Kati. Mafuriko hayo yaliyosababishwa na kuongezeka kwa ujazo wa mto Tobol karibu na mji wa Kurgan kusini mwa Urusi yamefikia viwango vya juu vya tahadhari.

Maafa hayo yamesababishwa na kuyeyuka haraka kwa theluji huku kukiwa na mvua kubwa, jambo linalosababisha kuongezeka kwa ujazo wa mito mikubwa zaidi barani Ulaya. Nchini Urusi karibu watu 200,000 wamehamishwa pia kutokana na mafuriko hayo.