Chelsea na Barcelona wamenyana Nou Camp. | Michezo | DW | 31.10.2006
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Chelsea na Barcelona wamenyana Nou Camp.

Ligi ya mabingwa barani ulaya inarejea tena leo usiku katika viwanja mbalimbali.

Kombe la mabingwa wa bara ulaya.

Kombe la mabingwa wa bara ulaya.

Majogoo wa Ujerumani Werder Bremen na Bayern Munich wanacheza usiku huu. Lakini macho yote yanaelekezwa Nou Camp, kwa mpambano kati ya mabingwa watetezi Barca na Chelsea…

Werder Bremen walio kileleni mwa ligi ya Bundesliga hapa Ujerumani wana kibarua chepesi watakaposafiri kwenda Bulgaria kwa mpambano na Levski Sofia…

Timu hiyo ya Bulgaria inaburuza mkia katika kundi la A bila ya pointi yeyote.

Bremen ambao wanaonekana kuwa katika hali nzuri kisoka wanatarajiwa kushinda pambano hilo.

Nao mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakichagizwa na ushindi wao mwishoni mwa juma katika ligi ya Bundesliga dhidi ya Hamburg,watakuwa nyumbani Munich kukutana na Sporting Lisbon.

Bayern wanaingia uwanjani, huku ikiwa bado hawajafungwa bao lolote.

Mechi nyingine usiku huu, ni huko Anfield kati ya mabingwa wa mwaka 2004 Liverpool na Bordeau, Roma wana miadi na wagiriki Olympiakos, Huku Spartak Moscow wakikutana na Intermilan.

Psv ya Uholanzi watakuwa nyumbani kuwaalika dim bani waturuki Galatasarray.

Lakini yote tisa kumi ni huko Nou Camp, asiye na mwana aeleke jiwe, pale mahasimu wawili Barcelona na Chelsea watakapoumana

Timu ya Frank Rijkaard ina kibarua kigumu baada ya kuonyeshwa kivumbi Stamford Bridge wiki mbili zilizopita ilipochapwa bao 1-0.

Goli la MuIvory Coast Didier Drogba liliwaacha mabingwa hao wa Ulaya na majogoo wa Uhispania wakitapatapa …na leo itawabidi wawanoe washambulizi wao kwani bila ya pointi tatu dhidi ya Chelsea huenda wakautema ubingwa.

Ingawa Barca watakuwa bila ya nyota yao, Mkamerron Samuel Eto, matumaini yao ya kuilipiza kisasi dhidi Chelsea, yanachigizwa na ushindi wao mwishoni mwa wiki katika la liga.

Chelsea na Barca wanakutana kwa mara ya sita sasa katika miaka mitatu, huku kila mmoja akipania kutoa mfano kuwa ndiye ngangari barani ulaya.

Ikumbukwe ya kwamba,msimu uliopita kwa timu kuweza kufuzu kwa raundi ya mtoano iliilazimu angalau kupata pointi saba tu, lakini msimu huu vilabu 9 tayari zimeshapitisha pointi hizo.

Sasa Vilabu 11 vinauwezo wa kuingia katika duru ya pili ya mtoano kwenye michezo itakayochezwa leo na kesho, hali inayoifanya ligi ya mwaka huu kuwa ya ushindani mkubwa.

 • Tarehe 31.10.2006
 • Mwandishi Munira Muhammad
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHd1
 • Tarehe 31.10.2006
 • Mwandishi Munira Muhammad
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHd1