Myanmar yakamilisha awamu ya mwisho ya uchaguzi mkuu
25 Januari 2026
Matangazo
Chama hicho "The Union Solidarity and Development Party" (USDP) kilichosheheni maafisa wastaafu wa jeshi kilishinda kwa asilimia 85 katika uchaguzi wa baraza la wawakilishi na theluthi mbili katika bunge, kwenye awamu mbili za awali
Wakosoaji waulalamikia uchaguzi
Wapiga kura kwenye miji 60 wanashiriki zoezi hilo katika miji mikubwa ikiwemo Yangon na Mandalay. Wakosoaji hata hivyo wanasema uchaguzi katika taifa hilo si huru wala wa haki na unalenga kuhalalisha mamlaka ya kijeshi ilisoiondoa serikali ya kiraia ya Aung San Suu Kyi Februari 2021.