1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Myanmar yafanya duru ya pili ya uchaguzi mkuu

Josephat Charo
12 Januari 2026

Myanmar imeanza duru ya pili ya upigaji kura jana Jumapili katika uchaguzi wake mkuu wa kwanza tangu jeshi lilipochukua madaraka miaka mitano iliyopita.

https://p.dw.com/p/56esu
Wapigaji kura walisubiri katika foleni kupiga kura zao huko Mandalay, katikati mwa Myanmar Jumapili Januari 11, 2026 katika duru ya pili ya uchaguzi mkuu.
Wapigaji kura walisubiri katika foleni kupiga kura zao huko Mandalay, katikati mwa Myanmar Jumapili Januari 11, 2026 katika duru ya pili ya uchaguzi mkuu.Picha: Aung Shine Oo/AP Photo/picture alliance

Upigaji kura uliongezeka hadi miji mingine ikiwemo baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali ya kijeshi na wapinzani wake wenye silaha.

Wakosoaji wanasema uchaguzi huo ulioandaliwa na serikali ya kijeshi si huru wala wa haki na ni juhudi za jeshi kuhalalisha utawala wake baada ya kunyakua madaraka kutoka kwa serikali iliyochaguliwa ya Aung San Suu Kyi mnamo Februari 2021.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo huru vya habari vya mtandaoni, ikiwa ni pamoja na Myanmar Now, mashambulizi yaliyolenga vituo vya kupigia kura na majengo ya serikali yaliripotiwa jana Jumapili katika angalau vitongoji vinne kati ya 100 vilivyokuwa vikiendesha vituo vya kupigia kura, huku maafisa wawili wa utawala wakiuawa.