Chama cha AfD kupata mafanikio katika uchaguzi wa Ulaya
2 Juni 2024Matangazo
Hayo ni kwa mujibu wa kura mpya ya maoni ya taasii ya INSA. Kama uchaguzi wa Ulaya ungefanyika Jumapili ya Juni 2, chama Mbadala cha Ujerumani, AfD kingepata asilimia 16 ya kura mbele ya chama cha Social Democratic (SPD) cha Kansela Olaf Scholz.
Muungano wa kihafidhina wa Ujerumani wa vyama vya Christian Democratic Union, CDU na chama cha Christian Social Union, CSU ulioneka kushika nafasi ya kwanza kwa asilimia 29 ya kura.
Kuelekea uchaguzi huo wa bunge la Ulaya, wakuu wa viwanda na vyama vya wafanyakazi nchini Ujerumani wameonya huenda kukawa na athari kubwa kwa taifa hili pamoja na uchumi wake iwapo Chama cha AfD kitapata mafanikio katika uchaguzi huo.