1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARACAS: Chavez na Morales wagombea urais Venezuela

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn5

Wapiga kura nchini Venezuela leo wanashiriki katika uchaguzi wa kumchagua rais mpya.Rais wa hivi sasa Hugo Chavez anaefuata siasa za mrengo wa kushoto na akiwa maarufu kwa kuikosoa serikali ya Marekani,anapigania kubakia madarakani kwa awamu ya miaka sita ijayo,ili kukamilisha mageuzi yake ya kijamaa.Mpinzani wake mkuu,mhafidhina Manuel Rosales alie gavana wa jimbo,anataka kuendeleza mfumo wa soko huru.Chavez anatazamiwa kushinda kwa sababu wapiga kura wengi walio masikini na wa tabaka la wafanya kazi wanaunga mkono mradi wake wa kupiga vita umasikini.Lakini hivi karibuni,idadi ya watu wanaomuunga mkono Rosales,imeongezeka na anaongoza upinzani ulio na umoja zaidi kulinganishwa na mwaka mmoja wa nyuma.