1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge Uganda lasimamisha vikao kusubiri jibu la Museveni

29 Agosti 2018

Bunge la Uganda limesitisha vikao vyake likimtaka rais Museveni atoe jawabu kuhusu madai ya wabunge kwamba askari waliowahujumu wabunge Bobi Wine na wengine wiki mbili zilizopita wakamatwe na kufunguliwa mashtaka.

https://p.dw.com/p/33wLu
Bunge la Uganda
Picha: DW/L. Emmanuel

J2 29.08 Uganda: Parliament suspended sitting - MP3-Stereo

Spika wa bunge Rebecca Kadaga alimwandikia barua rais Museveni kuhusu jambo hilo lakini hadi hapo bado hakuwa amewasilisha jibu. Badala yake rais Museveni aliwaita wabunge wa chama chake NRM na kuwashauri wasishiriki katika mjadala huo.