Brussels. Solana kukutana na Larijani. | Habari za Ulimwengu | DW | 20.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Brussels. Solana kukutana na Larijani.

Mratibu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana anatarajiwa kukutana na mjumbe wa ngazi ya juu wa Iran katika majadiliano ya kinuklia, Ali Larijani Jumatano ijayo.

Afisa wa umoja wa Ulaya mjini Brussels amesema kuwa watatumia mkutano huo kujadili iwapo itawezekana kurejea tena katika majadiliano kuhusiana na mpango wa Iran wa kinuklia.

Mahali pa kufanyia mkutano huo bado hapajapangwa.

Hapo mapema , shirika moja la habari la Iran liliripoti kuwa Larijani na Solana wamekubaliana kukutana wakati wa mazungumzo yao kwa simu siku ya Alhamis.

Hiyo ni moja kati ya mawasiliano kadha baina ya umoja wa Ulaya na Iran tangu baraza la usalama la umoja wa mataifa kuweka vikwazo vipya dhidi ya Tehran mwezi ulipita, kuhusiana na kukataa kwa nchi hiyo kusitisha shughuli zake za urutubishaji wa madini ya Uranium.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com