BERLIN : Wanajeshi wengine wanne wasimamishwa kazi | Habari za Ulimwengu | DW | 02.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Wanajeshi wengine wanne wasimamishwa kazi

Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imewasimamisha kazi wanajeshi wengine wanne kuhusiana na kashfa ya wanajeshi wa Ujerumani Bundeswehr waliopiga picha wakiwa na mabufuru ya binaadamu nchini Afghanistan.

Idadi hiyo inafanya idadi ya wanajeshi waliosimamishwa kazi hadi sasa kuhusiana na kashfa hiyo kufikia sita.Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Ujerumani amewaambia waandishi wa habari mjini Berlin kwamba zaidi ya wanajeshi 20 wanachunguzwa wengi wao wakiwa bado wanalitumikia jeshi la Ujerumani Bundeswehr.

Ujerumani ina takriban wanajeshi 2,800 wanaotumika kama sehemu ya kikosi cha Kimataifa cha Uzaidizi wa Usalama kinachoongozwa na kikosi cha Umoja wa Kujihami cha Mataifa ya Magharibi NATO nchini Afghanistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com