Baerbock akutana na mwenzake wa Misri kuhusu mzozo wa Gaza
25 Machi 2024Baerbock amekuwa akifanya kampeni kwa wiki kadhaa kwa ajili ya kusitishwa mapigano na kuachiwa mateka wa Israel wanoashikiliwa na kundi la Hamas hatua itakayowezesha misaada kufikishwa katika Ukanda wa Gaza.
Kabla ya safari yake ya Mashariki ya Kati, Baerbock alizitaka Israel na Hamas wafikie makubaliano ya kusitisha mapigano angalau ya muda mfupi.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa kupitisha azimio la kusitisha mapigano Gaza
Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajiandaa kupigia kura azimio la kushinikiza usitishwaji mara moja wa mapigano katika Ukanda wa Gaza ili kuruhusu kufikishwa misaada kwa Waislamu katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Azimio hilo la leo, limelowasilishwa na wajumbe 10 wa kuchaguliwa wa Baraza la Usalama na linaungwa mkono na Urusi na China pamoja na mataifa 22 ya Kiarabu kwenye Umoja wa Mataifa.