1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustralia

Baba na mwanawe wahusika mauaji ya Bondi Beach

15 Desemba 2025

Imefahamika kwamba washambuliaji waliowauwa watu 15 kwenye Ufukwe wa Bondi nchini Australia walikuwa baba na mwanawe wa kiume.

https://p.dw.com/p/55LKV
Australia Sydney 2025 | mashambulizi ya Bondi Beach
Waombolezaji wakibeba mashada ya mauwa kwenye msiba wa Bondi Beach, Australia.Picha: Mark Baker/AP Photo/picture alliance

Baba huyo mwenye umri wa miaka 50 aliuawa kwenye eneo la tukio baada ya kupigwa risasi na polisi, huku mwanawe mwenye umri wa miaka 24 akitiwa nguvuni baada ya kujeruhiwa.

Mashambulizi hayo ya jana yaliyolaaniwa na viongozi mbalimbali kama mashambulizi ya kigaidi, yalifanyika kwenye mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiadhimisha sikukuu ya Kiyahudi ya Hannukah.

Mwenye umri mdogo kabisa kuuawa kwenye mashambulizi hayo ya jana, Jumapili, alikuwa msichana wa miaka 10, aliyefia hospitalini, huku mwenye umri mkubwa kabisa akiwa mzee miaka 87.

Watu wengine 42 walijeruhiwa, wakiwemo maafisa wawili wa polisi. Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese, ametangaza bendera kupepea nusu mlingoti kuomboleza mauaji hayo.