You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Vita vya Marekani-Israel na Iran
Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola
Kombe la Dunia la FIFA 2026
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Wanepali wapiga kura mwaka mmoja baada ya kupinduwa serikali
Vituo vya kura vimefunguliwa nchini Nepal kwa uchaguzi wa kwanza tangu vijana kuiondowa serikali madarakani mwaka jana.
04.03.2026 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Iran imesogeza mbele maziko ya aliyekuwa Kiongozi wa Juu zaidi nchini humo Ayatollah Ali Khamenei / Urusi imeishtumu Ukraine kwa kutumia droni za majini kushambulia meli iliyobeba gesi ya asilia katika pwani ya Libya, na kusababisha kuzama kwake.
Mwangaza wa Ulaya: Mfumo wa kutoa tahadhari mtoto akipotea
Mfumo wa kipekee uliobuniwa miaka 20 iliyopita nchini Ufaransa ambao pia unatumiwa katika mataifa mengine ya Ulaya unaohusu kutoa tahadhari ya kitaifa pale kunaporipotiwa utekaji nyara wa watoto au hata taarifa ya mtoto kupotea. Miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, mfumo huu unaofahamika kwa kiingereza kama "Child abduction alert" umeendelea kutoa matokeo chanya katika suala zima la kuwalinda watoto.
04.03.2026 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mashambulizi ya anga ya Israel na Marekani dhidi ya Iran yameongezeka wakati kukiwa hakuna dalili ya vita kumalizika / Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, maporomoko mapya ya tope yamepiga chanzo cha sekta ya kimataifa ya coltan na kusababisha vifo vingi.
Upendeleo wa kijinsia wa AI katika Tafsiri za Kiswahili
Tafsiri za teknolojia ya akili mnemba AI hubeba pia mitazamo ya kijamii ikiwemo upendeleo wa kijinsia.
Vita vya Mashariki ya Kati vyaingia siku ya tano
Mashambulizi ya anga ya Israel na Marekani dhidi ya Iran yameongezeka wakati kukiwa hakuna dalili ya vita kumalizika.
03.03.2026 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Marekani Donald Trump amesema taifa lake linao uwezo wa kuendelea na mashambulizi dhidi ya Iran kwa muda mrefu / Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameanzisha mradi wa kupokea na kuhifadhi mafuta katika Bandari ya Dar es salaam
03.03.2026 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais Donald Trump asema mashambulio ya Marekani dhidi ya Iran yanaweza kuendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja / Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz anatarajiwa kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump
Vita vyazidi makali kanda ya Mashariki ya Kati
Iran imesema iko tayari kwa vita vyake na Marekani na Israel kama vitadumu kwa muda mrefu.
02.03.2026 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul, amesema Berlin haitoshiriki mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran / Jeshi la Marekani limesema ndege zake tatu za kivita ziliangushwa kimakosa kwa kushambuliwa na Kuwait
02.03.2026 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Israel na Iran zimeanzisha mashambulizi mapya dhidi ya kila upande / Mapigano kati ya Pakistani na Afghanistan
Matangazo ya Jioni: 28.02.2026
Iran imetishia kujibu vikali mashambulizi ya Marekani na Israel. Umoja wa Mataifa walaani vurugu zinazoshuhudiwa huko Mashariki ya Kati. Ufaransa yamhukumu Muhayimana miaka 14 jela kwa kushiriki mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
28.02.2026: Matangazo ya Mchana
Marekani na Israel zaishambulia Iran ambayo pia imeanza kujibu mapigo. Umoja wa Afrika watoa wito wa kupunguza haraka mvutano baada ya Marekani na Israel kuishambulia Iran. Serikali ya Ghana yatangaza kuwa raia wake 55 waliuawa baada ya kurubuniwa kujiunga na jeshi la Urusi kupigana vita nchini Ukraine.
27.02.2026 Matangazo ya Jioni
Juhudi za kuepusha vita kati ya Iran na Marekani zinaendelea, ambapo waziri wa mambo ya nje wa Oman+++Maelfu ya watanzania leo wamejitokeza katika ibada ya heshima ya kuuaga mwili wa Mwadhama Polycaro Kardinali Pengo, askofu mstaafu wa kanisa katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam.
Pakistan yaanzisha 'vita kamili' dhidi ya Afghanistan
Pakistan imetangaza vita kamili na vya wazi na Afghanistan kufuatia miezi kadhaa ya mashambulizi baina yao.
Afghanistan yapoteza wanajeshi 13 mashambulizi ya Pakistan
Ndege za kijeshi za Pakistan zilikuwa zinaendelea kuruka kwenye anga la Afghanistan.
Afrika CDC yaonya kuhusu mikataba ya afya na Marekani
Marekani inataka mataifa ya Afrika kutoa data zake za vimelea vinavyosababisha milipuko kabla ya kupata ufadhili.
27.02.2026 Matangazo ya Mchana
Pakistan imeishambulia kwa mabomu miji kadhaa ya Afghanistan, ukiwemo mji mkuu Kabul+++Wizara ya elimu nchini Kenya imechukua hatua dhidi ya wasimamizi wa shule 20, baada ya ripoti ya ukaguzi kufichua kuwepo kwa wanafunzi hewa zaidi ya laki tisa.
27.02.2026 Matangazo ya Asubuhi
Serikali ya Zambia imekataa kutia saini sehemu ya makubaliano ya mkataba wa msaada wa Marekani wa zaidi ya dola bilioni 1 kwa ajili ya kuipiga jeki sekta ya afya nchini humo+++Iran na Marekani zipo katika duru ya tatu ya mazungumzo mjini Geneva, Uswisi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Taarifa ya Habari za Asubuhi
Matangazo ya Asubuhi
Matangazo Mubashara
Matangazo mubashara kwa Kiswahili, Kihausa, Kiamharic, Kifaransa, Kireno na Kiingereza.
26.02.2026 Matangazo ya Jioni
Iran na Marekani zimeanza duru ya tatu ya mazungumzo leo Alhamisi mjini Geneva, Uswisi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran+++Shambulizi la droni la wiki hii lililomuua msemaji wa kundi la waasi wa M23 Willy Ngoma mashariki mwa Kongo, lilisababisha vifo vya watu wengine wanane
26.02.2026 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mvutano kati ya Marekani na Iran umefikia hatua nyeti huku pande hizo mbili zikikutana mjini Geneva / Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amewaambia wabunge wa Israel mjini Jerusalem kwamba nchi yake inasimama imara na Israel
26.02.2026 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Serikali ya Kenya imetangaza nia yake ya kuufungua mpaka wake na Somalia / Zimbabwe imejiondoa kwenye mazungumzo na Marekani kuhusu mkataba wa pamoja wa masuala ya afya kwa kuhofia ukiukaji wa sheria za kukusanya data
25.02.2026 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amewasili Israel / China na Ujerumani zimesisitiza umuhimu wa majadiliano yanayozingatia uwazi, ushindani wa haki na kuhakikisha upatikanaji wa masoko wenye usawa kati ya pande hizo mbili
25.02.2026 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Marekani Donald Trump amesema anapendelea kuutatua mzozo kati ya nchi yake na Iran kwa njia ya za kidiplomasia / Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz yuko nchini China kwa ziara yake ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa Kansela
Mahojiano: Je, Trump ameamua kuishambulia kijeshi Iran?
Mchambuzi Ibrahim Rahbi anafafanuwa kilichomo kwenye kitisho cha Trump dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
25.02.2026 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Marekani Donald Trump ametoa hotuba kuhusu hali ya taifa mbele ya Bunge la Marekani / Kansela Friedrich Merz wa Ujerumani anafanya ziara nchini China
25.02.2026 Taarifa ya Habari Asubuhi
Rais Trump asema Marekani sasa ni imara zaidi kuliko hapo awali // Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa latoa wito wa kusitishwa mapigano nchini Ukraine // Na Msemaji wa kundi la waasi wa M23 auawa mashariki mwa Kongo.
24.02.2026 Matangazo ya Jioni
Katika kumbukumbu ya miaka minne tangu uanze uvamizi wa Urusi dhidi Ukraine hivi leo, Urusi yakiri malengo yake Ukraine hayajafikiwa+++Mahakama kuu nchini Uganda imeahirisha kuendeshwa kwa kesi ya uhaini dhidi ya mwanasiasa wa upinzani Dokta Kizza Besigye+++Wakenya 600 waliokwama Cambodia waomba kurudishwa nyumbani
Urusi yakiri malengo yake Ukraine hayajafikiwa
Urusi imekiri malengo yake bado hayajafikiwa nchini Ukraine lakini imeapa kuendelea na vita hadi hapo itakapoyatimiza.
24.02.2026 Matangazo ya Mchana
EU yashindwa kukubaliana kuhusu vikwazo vipya vya Urusi huku vita vikiingia mwaka wa nne+++Rais Donald Trump atahadharishwa dhidi ya kuivamia Iran kijeshi+++Trump akanusha taarifa za onyo kuhusu kuishambulia Iran+++Takriban watu 74 wamekufa kufuatia machafuko nchini Mexico+++Amnesty International Kenya - Uchunguzi huru ufanyike kubaini waliomteka Mshabaha Hamza
Ukraine yafanya kumbukumbu ya miaka 4 ya vita vya Urusi
Zelensky ameapa kamwe nchi yake haitausaliti muhanga wa watu wake wanaokabiliana na Urusi.
24.02.2026 Taarifa ya Habari Asubuhi
EU yashindwa kukubaliana kuhusu vikwazo vipya vya Urusi huku vita vikiingia mwaka wa tano // Mexico yatuma wanajeshi 10,000 kukomesha ghasia kufuatia kifo cha El Mencho // Na Amnesty International yasema mwanaharakati wa Tanzania alitekwa nyara kabla ya kuokolewa Kenya
23.02.2026 Matangazo ya Jioni
Iran imesema leo kwamba uvamizi wa kiwango chochote utakaofanywa na Marekani utaifanya Jamhuri hiyo ya Kiislamu kujibu "vikali"+++Chama cha Wananchi CUF- cha nchini Tanzania kimepata uongozi mpya baada mkutano mkuu wa dharura kufanyika na kumuondoa Profesa Ibrahim Lipumba aliyekiongoza chama hicho kwa miaka 27.
23.02.2026 Matangazo ya Mchana
Hali ya usalama inaendelea kuwa ya kutisha katika wilaya ya Masisi nchini Kongo+++Wakati vita vya Urusi na Ukraine vikiingia mwaka wake wa nne, Rais Volodymyr Zelensky asema anaamini Rais Vladimir Putin wa Urusi tayari ameanzisha Vita vya Tatu vya Dunia.
23.02.2026 Matangazo ya Asubuhi
Sikiliza matangazo yetu ya asubuhi na miongoni mwa yale utakayosikia ni Taarifa ya Habari ya Ulimwengu, pamoja na makala za Vijana Tugutuke, Makala yetu Leo na Jukwaa la Manufaa.
Zelensky: Putin ameanzisha Vita vya Tatu vya Dunia
Asema nchi yake haitakuwa kikwazo cha kupatikana amani kwenye duru nyengine ya mazungumzo yanayosimamiwa na Marekani.
23.02.2026 Taarifa ya Habari Asubuhi
Mazungumzo ya Iran na Marekani yatarajiwa Alhamisi wiki hii licha ya hofu ya mashambulizi // Kiongozi wa genge lenye nguvu la dawa za kulevya nchini Mexico auawa kwenye operesheni ya kijeshi // Na Sudan yaikosoa Uganda kwa kumkaribisha mkuu wa kikosi cha RSF
22.02.2026 Matangazo ya Mchana
Iran na Marekani njia panda kuhusu viwazo na makubaliano ya nuklia +++Mwakilishi wa bishara Marekani asema bado makubaliano ya kibiashara na mataifa mengine yako thabiti+++Kundi la IS lamkashifu Al Sharaa kwa kumuita kibaraka wa Trump.
22.02.2026 Matangazo ya Mchana
Mataifa ya kiislamu na kiarabu yakosoa matamshi ya Huckabee kuhusu eneo la Mashariki ya Kati+++Trump apandisha ushuru hadi asilimia 15 kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani+++Urusi yanedelea na mashambulizi yake Ukraine.
Makala ya Afrika wiki hii
Suala la vijana wa Kiafrika kurubuniwa na kusafirishwa hadi Urusi ili kupigana vita nchini Ukraine. Tanzania ilisema kuwa vurugu zilizoshuhudiwa nchini humo wakati wa uchaguzi ni miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika mkutano wa marais wa Umoja wa Afrika. Na makabiliano yaendelea kuripotiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya miito ya usitishwaji mapigano.
Iran yashikilia msimamo idadi ya vifo vya waandamanaji
Iran imewataka wanaopinga takwimu za idadi ya vifo vya waandamanaji iliyotolewa na serikali watoe ushahidi.
20.02.2026 Matangazo ya Jioni
Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na misaada ya kibinadamu na usimamizi wa migogoro, Hadja Lahbib, yuko ziarani mjini Goma+++Serikali ya Urusi imejitenga na madai ya kuwasajili Wakenya wanaojiunga na jeshi lake katika vita vyake dhidi ya Ukraine
20.02.2026 Matangazo ya Mchana
Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo amefariki dunia jana usiku katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam+++Vyanzo vya Marekani vimesema huenda maeneo machache ya kijeshi au ya kiserikali ya Iran yakashambuliwa hivi karibuni.
19.02.2026 Matangazo ya Jioni
Mwezi mmoja baada ya kutiwa saini Mkataba wa Bodi ya Amani katika hafla yenye shamrashamra nyingi mjini Davos, Uswisi, Rais Donald Trump wa Marekani amewaalika wanachama wote wa bodi hiyo mjini Washington++++Mkutano wa kimataifa wa Akili Mnemba unafanyika New Delhi, India, ukiwaleta pamoja wakuu wa mataifa, wakurugenzi wa makampuni makubwa ya teknolojia na wawekezaji.
19.02.2026 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki nchini Iran Mohammad Eslami amesema hakuna nchi inayoweza kuinyima Jamhuri hiyo ya Kiislamu haki yake ya urutubishaji madini ya urani / Mahakama moja nchini Korea Kusini imemhukumu rais wa zamani Yoon Suk Yeol kifungo cha maisha jela
18.02.2026 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Marekani imeonya kwamba itaizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia "kwa njia moja au nyingine" / Hali ya wasiwasi imetanda kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia
18.02.2026 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Iran imetangaza kufungwa kwa muda kwa Mlango Bahari wa Hormuz / Waislamu na Wakristo wameanza rasmi misimu yao mikuu ya kiroho — Ramadhan na Kwaresma.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 8 wa 172
Ukurasa unaofuatia