1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Mlipuko waua sita Uturuki

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzL

Kumetokea mlipuko mkubwa wa bomu katikati ya mji mkuu wa Uturuki, Ankara ambapo watu sita wameuawa na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa.

Polisi wamesema kuwa bomu hilo lililipuka katika kituo cha basi katika eneo la kibiashara lenye watu wengi jijini Ankara.

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitembelea eneo hilo na kulaani shambulizi hilo.

Hakuna kundi lolote mpaka sasa lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini katika siku za nyuma, waasi wa kikurd, wanamgambo wenye mrengo wa kushoto na waislam wenye msimamo mkali, wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mabomu nchini Uturuki.

Mwezi Novemba mwaka 2003 zaidi ya watu 60 kutokana na mashambulizi ya mabomu katika mji wa Istanbul ambapo serikali ya nchi hiyo iliyahusisha na kundi la Al Qaida.