Ankara: Benedikti XV1 aanza ziara Uturuki leo | Habari za Ulimwengu | DW | 28.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ankara: Benedikti XV1 aanza ziara Uturuki leo

Kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki duniani Papa Benedikt XV1 leo anaanza ziara yake ya kwanza ya siku nne katika taifa la Kiislamu la Uturuki. Muda mfupi kabla ya kuanza ziara hiyo-ya kwanza katika taifa lenye waumini wengi wa Kiislamu, Kiongozi huyo mkuu wa kanisa katoliki duniani alisema ana matumaini italeta maelewano bora zaidi baina ya Wakristo na waislamu. Papa Benedikti XV1 kwanza ataelekea mji mkuu Ankara ambako kuna ulinzi mkali. Anatarajiwa kukutana na Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwenye uwanja wa ndege wa mji huo. Jumapili maelfu ya waturuki waliandamana mjini Istanbul kupinga ziara hiyo, baada ya Papa Benedikti kuzusha hasira miongoni mawa waislamu wengi duniani, kwa matamshi yake ya kuifungamanisha dini ya Kiislamu na matumizi ya nguvu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com