1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANC yazidi kupoteza uungaji mkono - Utafiti

24 Mei 2024

Utafiti wa maoni unaonesha chama cha African National Congress (ANC) kinachotawala nchini Afrika Kusini kinapoteza uungwaji mkono zikiwa zimebaki wiki tatu tu kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

https://p.dw.com/p/4gEXQ
 Cyril Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, ambaye chama chake cha ANC kinaelekea kupoteza uungaji mkono.Picha: Rodger Bosch/AFP/Getty Images

Kulingana na uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika la Social Research Foundation (SRF), chama cha ANC kimeshuka kutoka asilimia 45.9 hadi 40.9 ndani ya wiki moja tu, kufuatia maoni ya asilimia 60 ya wapiga kura.

Soma zaidi: Afrika Kusini yaadhimisha miaka 30 ya demokrasia

Hata hivyo, bado chama hicho, ambacho kimekuwa madarakani kwa miongo mitatu, kinapigiwa upatu kuibuka kuwa chama kikubwa katika uchaguzi huo wa Mei 29, lakini kwa mara ya kwanza, kinaweza kupoteza viti vingi bungeni.

Soma zaidi: Ramaphosa atafuta kura kwa Waafrika Kusini baada ya miaka 30 ya utawala wa ANC

Wiki iliyopita, Rais Cyril Ramaphosa alisaini sheria mpya inayolenga kutoa huduma ya afya kwa umma, licha ya pingamizi kutoka vyama vya upinzani na makundi ya wafanyabiashara.

Baadhi ya wachambuzi wanaamini hatua hiyo imechangia kuporomoka kwa uungwaji mkono wa chama.