1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

450,000 wana COVID-19, 7,000 wafa Afrika Kusini

Daniel Gakuba
28 Julai 2020

Visa vya maambukizi ya virusi vya korona nchini Afrika Kusini vinakaribia nusu milioni, huku idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa huo ikipindukia 7000.

https://p.dw.com/p/3g2Dd
Süfafrika Johannesburg | Covid-19 Impfstoff Tests beginnen
Picha: picture-alliance/AP Photo/S. Sibeko

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa nchi hiyo sasa imethibitisha maambukizi  452,529 ya ugonjwa huo, na jumla ya vifo 7,067, vikiwemo 300 vilivyorikodiwa kwa siku moja.

Afrika Kusini inayo nusu ya maambukizi yote ya virusi vya corona yaliyosajiliwa katika bara zima la Afrika, na inashikilia nafasi ya tano duniani.

Kama ilivyotokea kwingineko duniani, nchi hiyo imeshuhudia wimbi jipya la maambukizi baada ya kujaribu kuzifungua shughuli za kiuchumi.

Makampuni ya biashara yanalalamika, na kiwango cha wasio na ajira kimepanda hadi asilimia 30, kikitarajiwa kuendelea kuongezeka.