Zuma asema atashirikiana na Mbeki | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Zuma asema atashirikiana na Mbeki

POLOKWANE.Kiongozi mpya wa chama kinachotawala nchini Afrika Kusini cha ANC,Jacob Zuma amesema kuwa atashirikiana na Rais Thabo Mbeki katika kuendesha nchi.Zuma alimshinda Mbeki katika uchaguzi wa mwanzoni mwa wiki.

Akianisha agenda zake Zuma amesema chama hicho cha ANC kitaendelea na siasa na sera zake za zamani za kupambana na umasikini.

Ameongeza pia kwamba ataunga mkono mpango unaoleta utata wa mgawanyo wa ardhi.

Alisema hayo wakati wa kufunga mkutano mkuu wa chama hicho, muda mfupi baada ya kaimu mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ya Afrika Kusini kusema kuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha mahakamani Zuma kwa makosa ya rushwa.

Anatuhumiwa kuchukua hongo kutoka kwa kampuni ya silaha ya ufaransa ili kuisaidia kampuni hiyo kupata kandarasi ya kuiuzia silaha Afrika Kusini.

Zuma akijibu taarifa hiyo alisema kuwa atakuwa tayari kujizulu iwapo tuhuma hizo zitadhibitishwa na mahakama kuwa za kweli.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com