Ziwa Tanganyika
Tanganyika: Ziwa linalokalobiliwa na kitisho mwaka 2017
Ziwa Tanganyika
Mfuko wa Dunia wa mabadiliko ya Tabianchi, GNF umelitaja Ziwa Tangayika linalopitia Burundi, Jamhuri ya Kidemoktasi ya Kongo, Tanzania na Zambia kuwa ni Ziwa linalokabiliwa na kitisho kwa mwaka huu wa 2017. Kwa ushirikiano na taasisi mwenza inayosimamia ulinzi wa maziwa ya Bituraba, GNF imetaka kuweko kwa hatua endelevu za kulinda Ziwa hilo.
Uchafuzi: Kitisho kikuu
Uchafuzi wa mazingira, uharibifu uliopitiliza na kujaa kwa udongo kunaliweka Ziwa hilo la pili kwa ukubwa Afrika katika hatari kubwa. Taka za viwandani, ufundi na nyumbani kutoka maeneo ya karibu humwagika Ziwani vilevile zilivyo. Uchafuzi husababishwa pia na shughuli za usafirishaji pamoja na wavuvi wanaotumia mafuta kuendeshea jenereta na kuwasha taa, ambazo huzitumia kuvua nyakati za usiku.
Asilimia 17 ya dunia ni maji baridi
Likiwa na ukubwa wa mita 1,470, Tanganyika ni Ziwa lenye kina kirefu zaidi duniani na la pili kwa ukubwa wa maziwa yenye maji baridi. Lina angalau asilimia 17 ya maji baridi duniani. Kwa maana hiyo Ziwa hilo lina umuhimu kitaifa na kimataifa na chanzo cha riziki kwa mamilioni ya watu. Ni ziwa refu duniani, likiwa na Kilomita 673.
Nchi zinazotumia Ziwa hilo na ongezeko la idadi ya watu
Ikiwa ni kutokana na kuongezeka kwa shughuli zitokanazo na ongezeko la idadi ya watu kutoka nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Tanzania na Zambia, bonde la Ziwa Tanganyika sasa linakabiliwa na changamoto mbalimbali. Moja ya kumi ya watu Milioni 10 wanaoishi karibu na Ziwa hilo hutegemea moja kwa moja rasilimali za uvuvi za Ziwa hilo. Kiasi ya watu 100,000 miongoni mwao ni wavuvi.
Una Bayoanuwai muhimu
Ziwa Tanganyika ni makaazi kwa zaidi ya mimea 1,500 na aina za wanyama ambao, asilimia 40 ni adimu. Hii ina maana kwamba hawawezi kupatikana kwingine kokote duniani. Viumbe wakubwa, samaki aina ya Yavuyavu wanaoishi kwenye maji baridi na samaki aina ya Spinny eels ni mifano ya viumbe wanaoishi kwenye ziwa hilo, lakini pia mamba wa Mto Nile.
Uharibifu kupitia shughuli za uvuvi
Uharibifu wa rasilimali za Kibaiolojia unatishia Ziwa Tanganyika. Uvuvi uliopitiliza unapelekea kupungua kwa idadi ya samaki kwa kiwango kikubwa. Kati ya mwaka 1995 na 2011, idadi ya wavuvi imeongezeka mara nne zaidi, wakati ambapo idadi jumla ya samaki waliosalia imepungua kwa asilimia 25. Wakati huohuo, uvuvi kulingana na mvuvi mmoja mmoja kwa mwaka umepungua kwa asilimia 81
Kuzungumzia changamoto za mazingira
Profesa Pius Yanda, mtaalamu wa Jiografia ya eneo ambae pia ni Mkurugenzi mkuu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, " Suala muhimu zaidi ni kufanya kazi pamoja na kuona ni kwa namna gani tunaweza kuzizungumzia changamoto zinazoweza kutishia ikolojia. Kama watu watashiriki kikamilifu kuzizungumzia changamoto za kimazingira kwenye Ziwa hilo, litakuwa suala muhimu
Kusaka suluhu
Kunahitajika kupunguzwa kwa uchafuzi na matope. Lakini pia watu wa eneo hilo wanatakiwa kueleweshwa kuhusu sababu za matatizo wanayokutana nayo kila siku. Na muhimu zaidi, ni kuimarishwa kwa rasilimali mbadala za kujitafutia riziki. Miradi kama ya Bayoanuwai ya Ziwa Tanganyika inalenga kuzisaidia nchi zinazotumia Ziwa hilo kusimamia mfumo imara wa kulinda Biyoanuai ya Ziwa hilo.