Zapatero akataa kukutana na Kagame | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 17.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Zapatero akataa kukutana na Kagame

Maziri mkuu wa Hispania amekataa kuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa pamoja na rais wa Rwanda Paul Kagame mjini Madrid.

default

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa , Ban Ki Moon, akishikana mkono na rais wa Hispania Jose Luis Rodriguez Zapatero.

Waziri  Mkuu  wa  Hispania  amekataa  kuhudhuria mkutano  wa  Umoja  wa  Mataifa  pamoja  na  Rais  wa Rwanda  Paul  Kagame  mjini  Madrid  baada  ya  upinzani kutoka  kwa   wanaharakati  wa  haki  za  binadamu. Waziri Mkuu  Jose Luis  Rodriguez  Zapatero  alitarajiwa  kukutana na  Kagame  pamoja  na  katibu  mkuu  wa  umoja  wa mataifa  Ban Ki-Moon  kwa  ajili  ya  kikao  cha   kundi  la watetezi  wa  malengo  ya  maendeleo  ya   milenia. Lakini vyama  vya  upinzani   pamoja  na  makundi  ya  haki  za binadamu  yalimtaka  Zapatero  kutohudhuria  kwa sababu ya  kesi  zilizoko  mahakamani  nchini  Hispania   dhidi  ya maafisa  40  wa  Rwanda  wanaohusishwa  na  mauaji  ya kimbari  ya  mwaka  1994. Waziri  wa  mambo  ya  kigeni Miguel  Angel  Moratinos  alichukua  nafasi  ya  Waziri Mkuu  Zapatero, na  mkutano  huo  ulihamishwa  kutoka makao  rasmi  ya  serikali  na  kufanyika  katika  hoteli  mjini Madrid.

 • Tarehe 17.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/ONsP
 • Tarehe 17.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/ONsP
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com