1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Wizara ya afya Gaza yasema vifo kutokana na vita ni 32,845

1 Aprili 2024

Wizara ya Afya ya Gaza inayoongonzwa na Kundi la Hamas imesema leo kuwa watu wasiopungua 32,845 wameuawa katika eneo hilo kutokana na vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

https://p.dw.com/p/4eJtW
Uharibifu wa jengo baada ya shambulio la angani la Israel
Uharibifu wa jengo baada ya shambulio la angani la IsraelPicha: Khaled Omar/Xinhua/picture alliance

Idadi hiyo inajumuisha vifo visivyopungua 63 katika muda wa saa 24 zilizopita imesema taarifa ya wizara hiyo na kuongeza kuwa watu 75,392 wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita, vilivyochochewa na shambulio la Hamas ndani ya Israel mnamo Oktoba 7 mwaka jana.

Idadi ya vifo vya leo imetolewa saa kadhaa baada ya jeshi la Israel kuondoka kutoka hospitali kubwa zaidi ya ukanda huo ya Al-Shifaa, baada ya operesheni ya wiki mbili iliyoshuhudia mapigano makali.

Soma pia:  Jeshi la Israel laondoka katika hospitali ya Al-Shifa Gaza

Msemaji wa shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza, amesema leo kuwa vikosi vya Israel viliwaua karibu watu 300 ndani na karibu na hospitali hiyo katika wiki hizo mbili, huku Israel ikidai kwamba imewaua wanamgambo takribani 200.