1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Hatari ya virusi vya Hanta kwa umma ni ndogo

8 Mei 2026

Shirika la Afya Duniani WHO limesema hatari kwa umma kutokana na mripuko wa virusi hatari vya Hanta ni ndogo.

https://p.dw.com/p/5DV0J
Cape Verde, Praia 2026 | Uhamisho wa abiria wa meli ya utalii na wahudumu wa afya
Abiria watatu walioambukizwa wakiwa ndani ya meli MV Hondius wameshafarikiPicha: Misper Apawu/AP Photo/picture alliance

Kulingana na WHO, hatari ya kirusi hicho ni ndogo kwa umma kwa sababu virusi hivyo husambaa tu pale watu wanapokaribiana sana na walioambukizwa.

Mripuko huo wa virusi wa hanta uliotokea katika meli ya abiria MV Hondius, umezusha wasiwasi wa kimataifa.

Meli hiyo ipo njiani kuelekea kisiwa cha Tenerife nchini Uhispania. Tayari abiria watatu waliokuwa kwenye meli hiyo wameshafariki, huku WHO ikisema kuna watu watano ambao wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo na wengine watatu wanashukiwa kuambukizwa.

Msemaji wa WHO Christian Lindmeier amewaambia waandishi Habari mjini Geneva kwamba hatari ni ndogo kwani hata abiria wengine walikuwamo sehemu moja na walioambukizwa, hawaonyeshi dalili ya kuambukizwa.

Hata hivyo amesema kirusi hicho ni hatari kwa yule ambaye ameambukizwa.