Westerwelle awataka Wapalestina wazungumze na Waisraeli
27 Septemba 2011Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Ujeramani, Guido Westerwelle, amewatolea mwito Wapaletina warejee kwenye meza ya mazungumzo na Waisraeli kabla kudai taifa lao. Kwenye hotuba yake aliyoitoa katika Umoja wa Mataifa, waziri Westerwelle amesema Ujerumani inaunga mkono suluhisho la mataifa mawili, na kwamba imedhihirisha msimamo huo kupitia msaada wake kwa serikali ya mamlaka ya ndani ya Wapalestina. Kiongozi huyo aidha amesema taifa la Palestina linaweza tu kupatikana kupitia mazungumzo na viongozi wa Israel.
Rais wa mamlaka ya ndani ya Palaestina, Mahmoud Abbas, aliwasilisha rasmi ombi la uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa Ijumaa iliyopita na kuna uwezekano mkubwa ombi hilo likaidhinishwa katika baraza kuu la umoja huo. Hata hivyo Marekani inasema itatumia kura yake ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupinga ombi hilo kukiwa na haja ya kufanya hivyo.