1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza ziarani nchini Rwanda

19 Machi 2023

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman yupo ziarani mjini Kigali tangu jana Jumamosi ili kutetea mpango tata wa kuwahamisha hadi Rwanda waomba hifadhi wanaowasili nchini Uingereza.

https://p.dw.com/p/4Otnh
Großbritannien Innenministerin Suella Braverman
Picha: Kin Cheung/AP/dpa/picture alliance

Braverman ametembelea eneo la Bwiza kunakojengwa kituo cha kuwapokea wahamiaji hao na kusema makubaliano kati ya Uingereza na Rwanda yatasaidia kutafutia suluhu ya haki na kibinaadamu katika suala la wahamiaji.

Kigali na London walifikia makubaliano ya dola milioni 146. Mwaka jana, zaidi ya wahamiaji 45,000 waliwasili kwenye pwani ya Kusini-Mashariki mwa Uingereza wakitumia mashua ndogo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 60 kila mwaka tangu mwaka 2018.

Soma pia: Kagame na Sunak wazungumzia mkataba juu ya wahamiaji

Serikali na Upinzani nchini Uingereza wamekuwa wakitofautiana juu ya mpango huo ambao unaweza kuamuliwa kwenye Mahakama ya Juu ya Uingereza  baadaye mwakani. Hadi sasa, mpango huo haujaanza kutekelezwa.