1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa jimbo la Ujerumani ahimiza usalama zaidi wa mipaka

Tatu Karema
23 Desemba 2023

Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Brandenburg nchini Ujerumani Michael Stübgen, amesema anaamini mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya inapaswa kulindwa zaidi

https://p.dw.com/p/4aWRp
Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Brandenburg Michael Stübgen
Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Brandenburg Michael StübgenPicha: Soeren Stache/dpa-Zentralbild/picture alliance

Stübgen, ameliambia shirika la habari la dpa kwamba "ikiwa mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya itakuwa wazi na kuwalazimu kuwaruhusu watu zaidi kuingia kutokana na taratibu za mpaka, hali itazidi kuzorota.

Stübgen anatarajiwa kuchukua uenyekiti wa mikutano kati ya mawaziri wa mambo ya ndani wa majimbo 16 ya Ujerumani kuanzia mwezi Januari.

Soma pia:Austria ,na Ujerumani zafungua mipaka yao kwa wakimbizi

Mataifa ya Umoja wa Ulaya na Bunge la Ulaya yalikubaliana kuhusu taratibu za viwango sawa katika mipaka ya nje ya Umoja huo.

Mpango huo unatarajiwa kuwachukulia kwa umakini zaidi watu kutoka nchi ambazo zinazingatiwa kuwa

salama kiasi.