1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMashariki ya Kati

Waziri Mkuu wa Israel akutana na mrithi wa ufalme wa Bahrain

Iddi Ssessanga
15 Februari 2022

Waziri Mkuu wa Israel Naftal Benett amekutana na mrithi wa ufalme wa Bahrain, wakati ambapo washirika hao wapya wakilenga kujenga ushirikiano wa karibu na umoja dhidi ya adui yao wa pamoja Iran.

https://p.dw.com/p/4743p
Bahrain | Besuch israelischer Premierminister Naftali Bennett in Manamah
Picha: Dan Williams/REUTERS

Waziri Mkuu Bennet alikuwa katika ziara ya siku moja kwenye taifa hilo la Kifalme la kanda ya Ghuba, ambayo ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Israel, chini ya miaka miwili tangu mataifa hayo yalipoanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia.

Waziri Mkuu Bennet alipokelewa na mrithi wa kiti cha Ufalme, Salman bin Hamad Al-Khalifa, ambaye pia anahudumu kama waziri mkuu wa falme hiyo, na gwaride la kijeshi kwenye kasri la Gudaibiya mjini Manama.

Soma pia: Bahrain, UAE zaweka mahusiano ya kidiplomasia na Israel  

Amemumbia mwanamfalme Al-Khalifa kwamba amekuja kwa moyo wa ushirikiano, na kusimamo pamoja dhidi ya changamoto za pamoja.

Bahrain | Besuch israelischer Premierminister Naftali Bennett in Manamah
Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennet akikaribishwa na waziri wa mambo ya nje wa Bahrain Abdullatif bin Rashid Al Zayani katika uwanja wa ndege wa kimataifa ya Manama, Februari 14, 2022.Picha: Ilan Ben Zion/AP Photo/picture alliance

"Nataka kuwahsukuru marafiki zangu kwa makaribikisho mazuri. Kama mnavyojua, nakuja hapa kwa ziara ya kwanza rasmi ya waziri mkuu wa Israel nchini Bahrain.

Lakini ziara hii siyo tu ya kiishara. Lengo langu wakati wa ziara hii ni kuweka maudhui katika mikataba ya Abraham, katika biashara, katika miunganiko ya watu na watu na katika kila nyanja," alisema Bennet.

Bennett pia amekutana na mawaziri kadhaa wa serikali ya Bahrain na kujadili haja ya kushirikiana zaidi kiuchumi. Katika miezi ya karibuni, wakati mzozo na Iran ukiongezeka, mataifa hayo mawili yameimarisha ushirikiano wa kijeshi.

Mapema mwezi huu, yalisaini makubaliano ya kijeshi, na wiki iliyopita, Bahrain ilitangaza kwamba afisa wa jeshi la majini la Israel atawekwa mjini Manama, ambako pia ni nyumbani kwa kikosi cha tano cha jeshi la majini la Marekani.

Soma pia: Kwa nini mataifa ya Kiarabu yanakataa mahusiano na Israel

Israel na Bahrain zilianzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia baada ya miaka kadhaa ya ushirikiano wa siri wa kiuslama kuhusiana na uadui wao wa pamoja dhidi ya jirani yao Iran.

Flottenstützpunkt der USA in Bahrain
Baadhi ya meli za kivita za Marekani zilizoko Manama, Bahrain.Picha: MOHAMMED AL-SHAIKH/AFP/Getty Images

Mataifa hayo pia yamebadilishana mabalozi na kusaini makubaliano kadhaa ya biashara ya ulinzi tangu yaliposaini mikataba ya kuanzisha uhusiano, sambana na Umoja wa Falme za Kiarabu, Sudan, na Morocco mnamo Septemba 2020.

Ziara ya Benneti imekuja wakati majadiliano kati ya mataifa makubwa ya dunia na Iran, kufufua makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, yakiendelea mjini Vienna, Austria.

Israel inasema haitafungwa na makubaliano yoyote ya aina hiyo, na itachukuwa hatua wakati wowote itakapohitajika, ikiwemo mashambulizi ya kijeshi, kuizuwia iran kupata silaha za nyulia.

Chanzo: AP, RTRTV

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi