1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaDenmark

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen ashambuliwa

Lilian Mtono
8 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen jana Ijumaa alishambuliwa alipokuwa kwenye bustani ya Copenhagen, hii ikiwa ni kulingana na ofisi yake.

https://p.dw.com/p/4goBr
 Mette Frederiksen
Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen akiwa kwenye moja ya shughuli zake kabla ya kushambuliwa na mtu mmoja huko CopenhagenPicha: Jeremias Gonzalez/AP/picture alliance

Ofisi yake imeliambia shirika la habari la AFP kwamba Waziri Mkuu huyo alipigwa na mtu mmoja Ijumaa jioni katika eneo la Kultorvet mjini Copenhagen na kuongeza kuwa ameshtushwa na tukio hilo, ingawa haikueleza zaidi.

Imesema, mtu huyo hatimaye alikamatwa. 

Mkuu wa Umoja wa Ulaya Charles Michel pamoja na Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola wamelaani shambulizi hilo dhidi ya Frederiksen.

Tukio hili linatokea katikati ya ongezeko la mashambulizi dhidi ya wanasiasa wakiwa kazini ama kwenye kampeni nchini Ujerumani kabla ya uchaguzi wa wabunge wa Umoja wa Ulaya wiki hii.