1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCanada

Waziri Mkuu wa Canada Carney azuru China

14 Januari 2026

Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney amewasili mjini Beijing hii leo, tayari kuanza ziara ya siku nne inayokusudia kurekebisha uhusiano uliodorora kati ya mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/56oig
Mkutano wa G20-Johannesburg 2025 | Wakuu wa nchi na serikali wakiwa katika picha ya pamoja
Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney akiwa na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Na rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung Picha: Yves Herman/AFP

Canada inaangazia kuimarisha uhusiano na nchi nyingine, tofauti na Marekani.

Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa Canada nchini China katika kipindi cha karibu muongo mmoja. Carney atakutana na Waziri Mkuu Li Qiang pamoja na Rais Xi Jinping.

Carney ameitaja ziara hiyo ya China kama sehemu ya hatua za kujenga ushirika mpya kote ulimwenguni, ili kuhitimisha utegemezi wake kiuchumi kwenye soko la Marekani.

Licha ya Canada kuwa mshirika wa karibu wa Marekani kwa muda mrefu, Rais Donald Trump aliiwekea ushuru mkubwa kwa bidhaa zake zinazouzwa Marekani na kupendekeza kwamba taifa hilo lenye utajiri wa rasilimali linaweza kuwa jimbo la 51 la Marekani.