1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watatu wauawa Mandera

Mohammed Khelef
23 Juni 2017

Polisi nchini Kenya inasema washambuliaji wamewapiga risasi na kuwauwa watu watatu wakati wa uvamizi wa benki moja ya kibiashara kaskazini mashariki mwa nchi hiyo hivi leo.

https://p.dw.com/p/2fFfU
Kenia Sicherheitskontrollen an der Grenze zu Somalia 08.12.2014
Picha: Reuters/G. Tomasevic

Waliouawa ni raia wawili na afisa mmoja wa polisi katika mashambulizi hayo kwenye Kaunti ya Mandera, kwa mujibu wa kamanda wa polisi, Charles Chacha.

"Kulikuwa na majambazi watano wenye silaha. Walipofika kwenye benki, walimpiga risasi afisa wa polisi aliyekuwapo mlangoni, na polisi walifanikiwa kumpiga risasi mmoja wa wahalifu hao, lakini...walikimbia," Chacha aliliambia shirika la habari la Reuters.

Elwak, mahala hasa ambapo mashambulizi hayo yametokea, pako karibu na mpaka wa Somalia.

Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu linasema pia kuwa bomu lililotegwa barabarani limeripuka kwenye mji huo huo wa Mandera, ingawa hakuna taarifa za waliouawa ama kujeruhiwa kwenye mripuko huo.

Mandera imekuwa ikishuhudia mashambulizi ya mara kwa mara, ambayo yameangamiza maisha ya maafisa kadhaa wa usalama na raia wa kawaida. Kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye mafungamano na al-Qaida limekuwa likibeba dhamana ya mashambulizi hayo.

Mwandishi: Mohammed Khelef/Reuters
Mhariri: Saumu Yussuf